Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini kupitia CCM, Antony Mavunde akihutubia katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za jimbo hilo kwenye Uwanja wa Shule ya Chang'ombe, jijini Dodoma.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
WANANCHI waliopisha ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato Dodoma, Barabara za Ringroad, wataanza kulipwa fidia hivi karibuni.
Hayo yamesemwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anthony Mavunde wakati wa uzinduzi wa kampeni kwenye viwanja vya Shule ya Chang'ombe, jijini Dodoma Septemba 5, mwaka huu.
Mpango huo ulipokelewa kwa nderemo na vigelegele na wananchi waliohudhuria uzinduzi huo uliofurika umati mkubwa.
Taswira ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato Dodoma itakavyokuwa ukikamilika |
Amesema endapo akichaguliwa yeye, Mgombea Urais wa chama hicho, Dk. John Magufuli na madiwani 41 wa jimbo hilo, ameahidi kusambaza kompyuta katika shule zote za msingi na sekondari zilizomo jimboni humo.
Pia, Mavunde ameahidi kuandaa utaratibu wa kuwapatia mikopo wajasiriamali, wafanyabiashara ndogo ndogo, vijana, akina mama na walemavu.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Kibakwe, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Steven Masele, wagombea ubunge Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile na Fatma Toufiq. Wote hao walipata wasaa wa kmnadi Mavunde, Dk. Magufuli na madiwani wa CCM.
Wengine waliohudhuria kampeni hizo ni; viongozi wa chama, waliogombea ubunge kwenye kura za maoni na kushindwa, wagombea udiwani Kata 41 zilizomo kwenye Jimbo hilo na wageni wengine waalikwa.
Sehemu ya umati wa watu uliohudhuria uzinduzi huo wa kampeni
Post a Comment