Featured

    Featured Posts

MGOMBEA UBUNGE MAKOA AAHIDI KUTATUA TATIZO LA MAJI, KUBORESHA MIUNDOMBINU KONDOA

Mgombea Ubunge Jimbo la Kondoa Mjini, Ally Makoa (kulia) akiwa na Msimamizi wa Shughuli za Uchaguzi wa CCM Mkoa wa Dodoma na Mlezi wa CCM wa mkoa huo, Spika wa Bunge, Job Ndugai wakicheka kwa furaha baada ya Ndugai kumnadi katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za jimbo hilo, mjini Kondoa juzi.
Makoa akimwaga sera nzuri za Chama Cha Mapinduzi, wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Kondoa Mjini, kwa kuwataka wananchi ifikapo Oktoba 28, mwaka huu kumpigia kura yeye, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli na madiwani wa CCM.
Sehemu ya umati wa wananchi ukiwa katika mkutano huo wa kampeni.

Makoa akizungumza jambo na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini, Dk. Ashatu Kijaji.
Makoa akitoa ahadi kwamba akichaguliwa atafuatilia kero ya maji na kuitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Mke wa Makoa, Asha Habib akimuombea kura mumewe wakati wa kampeni hizo.

Makoa akiwa jukwaa kuu pamoja na viongozi mbalimbali
Wagombea Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma wakijitambulisha na kumuombe kura Makoa na Dk. Magufuli pamoja na madiwani wa CCM. Kutoka kushoto ni Halima Okash, Fatma Toufiq na Mariam Ditipile.

Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Mgombea wa Jimbo la Kondoa Mjini, Makoa akiwaomba kura.


Na Mwandishi Wetu, Kondoa.

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kondoa Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ally Makoa amesema endapo akichaguliwa, ameahidi kwanza kulitafutia ufumbuzi tatizo kubwa la maji jimboni humo.

Amesema kuwa kama Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 inavyoeleza kwa Kondoa Mjini, atafuatilia ujenzi wa matanki makubwa ya kuhifadhi maji na kuboresha miundombinu iliyojengwa miaka ya 70 wakati huo idadi ya wakaazi ikiwa ndogo.

Mgombea huyo, ameahidi pia kufuatilia usambazaji wa umeme vijijini ambapo atahakikisha unawafikia wananchi.

Pia, ameahidi kushughulikia uboreshaji wa miundombinu ya barabara vijijini na kujenga Daraja la Mto Munguri linalowatesa wananchi wakati wa masika.

 Amesema yote hayo yatafanikiwa iwapo tu wananchi watawapigia kura wagombea wa CCM wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana