CCM Blog,Tarime
MGOMBEA mahiri wa Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara ambaye pia ni Naibu Waziri TAMISEMI amesema akishachaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo miongoni mwa vipaumbele vyake vya kwanza itakuwa ni kuondoa na kukomesha kabisa ukabila katika jimbo hilo.
Waitara ameyasema jana Septemba 8, 2020, katika uzinduzi wa kampeni zake uliofanyika kijijini Nyamwaga na kuhudhuliwa na maelfu ya Watu.
Amesema mambo ya ubaguzi wa koo yanaleta ukabila jambo ambalo si zuri na hivyo akishachaguliwa kuwa Mbunge ataunganisha koo zote ili kuwa kitu kimoja.
Waitara ambaye mhula uliopita alikuwa Mbunge wa Ukonga kwa tiketi ya CCM amesema atahakikisha ana maliza vita baaina ya Wanyamongo na Wairege na kuhakikisha anafahamu chanzo na ni nani anayechochea ugonvi huo.
Akiendelea kuzungumza amesema atahakikisha anawaletea Wanyamongo maji safi na salama pamoja na barabara ya rami.
Ameongeza kuwa tayari kuna shiringi bilion1 za kujenga majengo ya Halmashauri ya Tarime Vijijini.
Waitara amesema Tarime pamoja na Serengeti ndiyo miji iliyobeba uchumi wa Mkoa wa Mara lakini Tarime ina miuundo mbinu mibovu hivyo akichaguliwa atahakikisha inaboreshwa.
Pia amesema kuwa maeneo yote ya kutoa huduma muhimu kwa jimbo lake yanahitaji ukarabati na kuongeza kuwa anaijua siasa vyeo atakutana navyo mezani.
Hata hivyo amesema ataweka mahusihano mazuri kati ya TRA Sirari pamoja na bodaboda ili kuondoa kero ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara na kusababisha usumbufu usio wa lazima.
Post a Comment