Featured

    Featured Posts

MPIGIENI KURA ZA TSUNAMI DK MAGUFULI-OKASH

Mgombea Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia CCM, Halima Okash akielezea sera na mafanikio ya ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mgombea Urais wa CCM, Rais Dk. John Magufuli,  alipokuwa akiwaombea kura wagombea wa CCM, akiwemo  Dk. Magufuli, Mgombea Ubunge Jimbo la Chemba, Mohammed Monni na Mgombea Udiwani wa Kata ya Soya, Mashaka Mashaka.

Okash (kulia) akiomba kura kwa unyeyekevu katika moja ya vikao vya ndani wilayani Chemba.



Sehemu ya viongozi wa CCM wa Kata ya Soya wakiwa katika Kikao cha Ndani kilichoongozwa na Okash.

Okash (wa pili kulia), akiwa na baadhi ya viongozi wa Umoja wa Wanawake (UWT).



Okash akiwa katika kikao cha ndani cha viongozi wa Kata ya Soya ambapo pamoja na mambo mengine walipanga mikakati ya kuhakikisha kura nyingi wanapigiwa wagombea wa CCM  

Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma, Okash akifanya kampeni katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Soya.

Na Mwandishi Wetu, Chemba

MGOMBEA Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Halima Okash amewaomba wananchi kumpigia kura za tsunami Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli Oktoba 28, mwaka huu, ili kumlipa wema kwa mambo makubwa aliyoifanyia Tanzania.

Okash alitoa ombi hilo kwa unyenyekevu huku akiwa amepiga magoti, alipofanya mikutano ya ndani na ya hadhara katika Kata ya Soya, wilayani Chemba, Dodoma.

"Msidanganyike kabisa na vyama vingine, kwani maendeleo yameletwa na CCM na yataendelea kutekelezwa na CCM. Tumlipe wema Dk. Magufuli aliyeifanyia mambo makubwa Tanzania kwa kumpigia kura za Tsunami Oktoba 28, 2020, kwani wema hulipwa kwa wema,"alisema Okash.

Akiwa katika kata hiyo, Okash alifanya vikao vya ndani kwa viongozi wa kata, vikao na wanawake na hatimaye kwenye mkutano hadhara ambapo alielezea mambo mazuri yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. Magufuli.

Alitumia fursa ya vikao hivyo kuwaombea kura pi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chemba, Mohammed Monni na Mgombea Udiwani wa Kata ya Soya, Mashaka Mashaka.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana