Featured

    Featured Posts

POLEPOLE: TUNDU LISU HATUMII DATA ANAPOZUNGUMZA NA KADAMNASI YA WATU, NI MWONGO MWANZO MWISHO

 

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Idara ya  Itikadi na Uenezi Hupmhrey Polepole akizungumza katika mkutano wake na Waandishi wa habari, uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, leo.

CCM Blog, Dodoma

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Idara ya  Itikadi na Uenezi Hupmhrey Polepole, amesema Mgombea Urais wa Chadema Tundu Lisu anamhisi kuwa ana matatizo katika uwezo wa kutunza vizuri kumbukumbu kichwani hali inayomfanya kutamka mambo ya uongo hasa anapokuwa kwenye kadamnasi ya watu.


Polepole amesema madai hayo huku akiushutumu viongozi wa Chadema, akisema inakuwaje viongozi hao wanamuacha mgombea wa chama chao anazungumza vitu vya uongo wakati takwimu na nyaraka zinazoeleza kila kitu kwa uwazi zipo.


Polepole ametoa madai hayo hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akieleza tathmini na mwenendo wa kampeni za Mgombea Urais wa CCM Rais Dk. John Magufuli, alipokutana na Waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete na kuongeza kusema, "kama huyu Lisu hajui mambo atuulize tumueleze lakini si kupita na kusema uongo".


“Nadhani huyu mtu kuna mahali hapako sawa kwenye kichwa chake, sitaki kunasabisha uwezo wake wa kutunza kumbukumbu na matatizo yaliyomkuta huko nyuma, lakini inasikitisha sana na kushangaza sana sana kuona mtu kama huyu anayetafuta kuongoza nchi kuwa muongo muongo kiasi hiki,” amesema Polepole.


Polepole amesema uamuzi wa Rais Dk. John Magufuli kununua ndege kweli ni uamuzi mgumu lakini akasema yeye siye wa kwanza kufanya hivyo duniani, akitolea mfano wa umuhimu wa kuanzisha mashirika ya ndege na uamuzi mgumu wa kununua ndege uliofanywa na aliyekuwa Mtawala wa Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mfalme Mohamed Bin Rashid Al Maktoum ambaye alimtaja akisema kuwa kiongozi huyo mwaka 2001 alifanya uamuzi mgumu wa kununua ndege 56 kwa wakati mmoja kwa ajili ya Shirika la Ndege la Emerates Airlines ambalo hadi sasa lipo na ni moja ya mashirika makubwa ya ndege Duniani.


"Al Maktoum alipata kusema kwamba hakuwahi kufanya uamuzi mgumu katika maisha yake kama huo wa kununua ndege 56 kwa mkupuo, lakini leo tunaona shirika la ndege linaloongoza kwa ukubwa duniani ni Emirates. Hivyo, hata Rais Magufuli kwa uamuzi wa kununua ndege wapo wanaombeza lakini watakuja kumkumbuka,” amesema Polepole.


Akizungumzia kuhuishwa kwa Shirika la Ndege (ATCL), ambapo alikumbusha kuwa hadi mwaka 2015/16 shirika hilo lilikuwa hoi  “Mpechempeche” kifedha, lilikuwa linatengeneza hasara huku likiwa na ndege moja tu tena mbovu na ya kukodi. Lakini ndani ya miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano zilinunuliwa ndege 11 ambapo hadi sasa ndege nane zimeshawasili.


Kingine alichogusia ni namna Lissu alivyosema ndege zilinunuliwa bila kuidhinishwa katika bajeti ya taifa, na kumbusha kutoka nukuu ya Kumbukumbu za Bunge (hansard) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinaonyesha jinsi kati ya Juni 2016 hadi Juni 2018 wabunge walivyokuwa wakijadiliana juu ya kununuliwa ndege na fedha zikatengwa.


Polepole amesema wapo wanaotumia kampeni za mwaka huu kuzungumza uongo na kuzua tafrani kuhusu viwanja vya ndege, na kusema kwamba suala la viwanja vya ndege si la eneo moja au la kumhusisha mtu bali ni la wananchi na kuleta maendeleo.


Ameitaja baadhi ya mikoa ambayo kuna viwanja vinavyokarabatiwa na vingine vinajengwa vipya ni pamoja na Dodoma, Singida, Mpanda, Chato, Tabora, Mtwara, Musoma pamoja na Shinyanga ambavyo alisema vimejengwa kimkakati wa kuchochea maendeleo na si vinginevyo.


Polepole amesema anashangazwa na Tundu Lissu anaposema Uwanja wa Ndege wa Mpanda ulijengwa kwa sababu ya Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda na sasa hautumiki, jambo ambalo si kweli kwani uwanja huo ulijengwa kwa ajili ya sababu za kiuchumi kwenye mkoa wa Katavi na unatumika akitoa ushahidi kwamba hadi juzi ndege ilitua kwanye Uwanja huo na abiria walio wengi kwenye ndege hiyo walikuwa watalii ambao hufika katika mkoa huo kwa ajili ya kwenda kutalii kwenye Hifadhi ya Taifa ya Katavi.


Kuhusu ujenzi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) unaoendelea kwa sasa kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora na baadaye hadi Mwanza umefanyiwa upembuzi yakinifu kuihuisha reli ya zamani ikiwemo kuiongezea uwezo reli ya kati na kuifufua reli ya Kaskazini.


“Reli ya kati tuliiongezea ratili ili iweze kubeba mizigo mizito na abiria wengi zaidi pamoja na kuiongezea kasi, ilikuwa na ratili 45 imepanda hadi 60. Itakuwa na uwezo wa kubeba mzigo mkubwa pamoja na kuwa na kasi inayofikia kilomita 70 kwa saa,” amesema Polepole.


Kuhusu mwenendo wa kampeni za CCM, Polepole alisema zimeendelea vizuri sana, na ari ya mgombea wa Urais Rais Dk. John Magufuli imezidi kuongrzeka huku hali ya afya yake ikiwa imara kuweza kuendelea na kampeni katika awamu ya mwisho.


"Ndugu Watanzania, kwa niaba ya Mgombea wetu, tunawashukuru sana kwa kumuombea Mgombea wetu afya njema na tunawashukuru zaidi kwa ari yenu ya kuwa mnajitokeza kwa wingi sana kwenye mikutano yetu, sasa tunawaomba mzidi kumuombea afya njema Dk. Magufuli na pia muendelee kuja kwa wingi kwenye mikutano yetu


Lakini pia tunawasihi ifikapo Oktoba 28, mwaka huu kila mmoja wetu ajitokeze na kuhakikisha anampigia kura ya ndiyo Dk. Magufuli, aibuke na ushindi mnono Chama Cha Mapinduzi kiwe kifua mbele na kuendelea kuwaongoza kwa umahiri mkubwa, nchi yetu isonge mbele zaidi", alimalizia Polepole.


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana