Na Lydia Lugakila, Bukoba
Mgombea Uras kw tiketi ya CCM, Rais Dk. John Magufuli anatarajiwa kuwasili mkoani Kagera siku ya Jumanne, Septemba 15, 2020 kuendelea na awamu ya pili ya Kampeni zake za kusaka kura kwa wananchi ili kuibuka na ushindi wa kishindo kwa kura nyingi atakazopata katika uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwishoni mwezi ujao.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Kagera Hamimu Mahamood amewaambia waandishi wa habari leo kwamba baada ya kuwasili Mgombea huyo wa Urais Dk. Magufuli atakutana na Wananchi katika maeneo mbali mbali na baadaye kuhutubia mkutano wa Kampeni katika Viwanja vya Gymkhana, vilivyopo katika Manispaa ya Bukoba.
Amesema Dk. Magufuli mbali na kuwaomba wananchi kuichagua CCM atazungumzia jinsi Serikali ya awamu ya tano anayoiongoza ilivyofanikiwa katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya 2015-2020 na namna gani CCM imejipanga kukamilisha au kufanya miradi mipya iliyoianisha katika Ilani yake ya Uchaguzi wa mwaka huu wa 2020.
Mahamood amesema, shesho yake, Septemba 16, 2020 ataondoka Bukoba mjini na kwenda Wila ya Muleba kuendelea na ziara yake ya kampeni katika mkoa huo wa Kagera.
Mwenezi huyo amewataka wana CCM na wananchi kwa jumla kujitopkeza kwa wingi ili kuweza kusikiliza wenyewe ya Mgombea wa Urais wa CCM Dk Magufuli atakayozungumza bada ya kusubiri kusimuliwa na hatimaye kuambiwa uwongo.
Post a Comment