Featured

    Featured Posts

SERIKALI YAWAJIBU WANAONUNG'UNIKA KWAMBA UNUNUZI WA NDEGE UMEFANYWA KWA SIRI


Msemaji Mkuu wa Serikali ambae pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Dr. Hassan Abbas ametoa majibu kuhusu manung’uniko ya ununuzi wa Ndege za AirTanzania kuwa umefanywa kwa siri na kusema “kwenye hii miaka mitano hakuna kitu ambacho hatujakieleza tunakifanya kwa sababu gani, Watu wameamua tu kujitungia stori zao haelewi Ndege zimenunuliwaje, kama ni uwazi umefanyika sana na wa kutosha”

“Ndege kuna utaratibu wa zabuni unafanyika, ukirudi kwenye sheria ya manunuzi ya umma ya Serikali modeli iliyotumika kununua Ndege zetu tumepeleka tenda ile kwa Makampuni yanayotengeneza Ndege yenyewe na sio kwenda kwa Wakala ambae ataweka cha juu chake, kwahiyo tulipohitaji Boeing tulikwenda kiwandani kwenyewe, Bombadier tulikwenda kiwandani Canada, sasa Watu wamepiga kelele sababu kuna mambo ya dili” – Dr. Hassan Abbas akiongea na Times FM.

Kuhusu ishu ya mikataba ya Madini kutopita Bungeni, Dr. Abbas kwenye Interview na BBC amesema “Kwenye sheria yetu ya mwaka 2017 imesisitiza na kuongeza ngazi nyingine za uwazi kwenye mikataba ya madini mfano huko nyuma Waziri wa Madini alikua anasaini tu mkataba lakini kwa sasa mikataba itakwenda mpaka kwenye baraza la mawaziri, itapita kwa Makatibu Wakuu, itapita kwenye Baraza Mawaziri wote watatoa maoni yao na ukisoma pia kwenye sheria za rasilimali za mwaka 2017 kumewekwa kipengele pale inapolazimika pia Bunge litapewa” – Dr. Abbas. 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana