Mgombea Urais wa Zanzibar Zanzibar kwa tiketi ya ACT- Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad, amekwaa kisiki na hivyo kushindwa kuanza kufanya kampeni baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kushindwa kumpitisha kutokana na kuwekewa pingamizi.
Maalim Seif atakuwa huru na kupitishwa na ZEC atakapofanikiwa kudadavua na kushinda pingamizi aliyowekewa kwa kujibu hoja zinazohusiana na pingamizi hiyo.
Maalim Seif amekwama huku ZEC ikiwa tayari imewapitisha wagombea 16 kati ya 17 waliomba kuteuliwa nafasi hiyo ya Urais na sasa wapo huru kuanza kufanya kampeni.
Post a Comment