Alodia Babara, Bukoba.
Meneja wa Mamlaka ya hali ya hewa mkoa wa Kagera steven Malundo amesema kuwa, mvua za vuli katika maeneo mbalimbali mkoani Kagera zinatarajiwa kuwa za wastani au chini ya wastani hivyo, wakulima wapande mazao ya muda mfupi yanayokomaa haraka na yanayoweza kustahimili ukame.
Aliyasema hayo jana wakati akiongea na gazeti hili juu ya matarajio ya hali ya mvua za vuli zitakazonyesha kuanzia septemba mwaka huu hadi januari mwaka kesho.
Aliongeza kuwa, mvua zinatarajia kuanza kunyesha wiki ya pili ya mwezi wa tisa ambapo mwezi wa kumi itanyesha wastani wa milimita 158, novemba itanyesha wastaniwa milimita 204na mwezi wa desemba itanyesha milimita 181 na kwa msimu mzima itanyesha wastani wa milimita 544 au zinaweza kuwa chini ya milimita hizo.
Alisema kutokana na mvua hizo kuwa za wastani na chini ya watani wakulima wapate ushauri kutoka kwa maafisa ughani ni mazao yapi wayapande.
Kwa upande wa baadhi ya wakulima walioongea na gazeti hili ambao ni Pastory Anatori na Aloyce Mpira walisema kuwa mvua zinapokuwa za wastani zimekuwa zikiwaathiri kwani zinaweza kunyesha maeneo na maeneo mengine zisinyeshe.
Pastory Anatory mkazi wa Minziro wilaya ya Misenyi alisema kuwa, anaenda kuandaa maharage na mahidi ambayo yanakomaa kwa muda mfupi ili aendane na hali ya hewa iliyotangazwa na mamlaka hiyo.
Naye Aloyce Mpira mkazi wa kata ya Kiruruma wilayani Karagwe alisema kuwa, zinaponyesha mvua za wastani maharage na mazao mengine yanastawi sana tofauti na mvua zinaponyesha nyingi hualibu mazao mashambani.
Post a Comment