Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru Ally Kakurwa akizungumza wakati akizindua mafunzo ya Mawakala wa CCM kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuelekea Uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28,2020
Baadhi ya Mawakala wakiwa katika uzinduzi wa mafunzo hayo
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM DK. Bashiru Ally wakati alipokuwa akizungumza nao na kuwashukuru viongozi wa dini kwa kuliombea taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli
……………………………………………………………………………….
Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru ally Kakurwa amezindua mafunzo ya mawakala wa CCM katika Uchaguzi Mkuu mkoa wa Mwanza na kueleza kuwa, mafunzo hayo sasa yanaendelea nchi nzima.
Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 16 Oktoba, 2020 katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
“Nimeamua kuja Mwanza kufanya kazi ya kuzindua mafunzo kwa viongozi wa Chama na mawakala wa uchaguzi kwa niaba ya Chama kwa sababu za kimkakati,”
Akisisitiza kwa viongozi hao na mawakala ameeleza kuwa, “Kwanza, Tumeshakubaliana na Mwenyekiti wa Mkoa kwamba hakuna jimbo lolote la mkoa wa Mwanza litakalotoka mikononi mwa CCM “
Aidha katika hatua nyingine Katibu Mkuu, ameshiriki ibada ya Ijumaa katika msikiti wa Mkoa wa Mwanza, ambapo ametumia fursa hiyo kutoa shukrani kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM na Mgombea Urais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa viongozi wa dini zote kuendelea kuhimiza amani na mshikamano wakati wote hasa tunapoelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 28 Oktoba, mwaka huu, na amewaomba, kuendelea kufanya hivyo bila kuchoka.
Hii ni ziara ya siku nne ya Katibu Mkuu na mlezi wa Mkoa wa Mwanza, ambapo kesho atakuwa katika wilaya ya Nyamagana.
Post a Comment