Featured

    Featured Posts

OKASH AZUNGUKA KATA 70 DODOMA KUPAMBANIA KURA ZA DK MAGUFULI



Okash akigawa picha za kampeni za Mgombea Urais wa CCM, Dk.John Magufuli katika Stendi Kuu ya Dodoma ikiwa ni moja ya mikakati yake ya kutafuta kura za wagombea wa CCM.


Mawakala wa uuzaji tIketi za mabasi wakifurahia kugawiwa na Okash  picha za Dk Magufuli  alipofanya kampeni katika Stendi Kuu ya Mabasi Dodoma.



 Okash akipiga magoti kuwaombea kura wagombea wa CCM.



Na Richard Mwaikenda, Dodoma

MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Halima  Okash hadi sasa amefanya kampeni kwa mafanikio ya kuzisaka kura za Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli zaidi ya kata 70 kwenye majimbo yote 9 ya mkoa huo.


Okash ambaye awali alipangiwa kufanya kampeni katika majimbo mawili ya Kondoa Vijijini na Mvumi, amevuka malengo kwa kuzitafuta kura za Dk Magufuli na wagombea wengine CCM katika majimbo yote 9. Majimbo mengine ni; Kongwa, Mpwapwa, Chamwino, Bahi, Dodoma Mjini na Kibakwe.


"Nimefikia Kata 70, vijiji 92 katika majimbo yote ya Dodoma. Nilipangiwa majimbo ya Kondoa Vijijini na Mvumi ambapo kwa Mvumi nimezifikia kata zote 22 na vijiji 45 na kwa upande wa Kondoa Vijijini tayari nimezifikia kata zote 21 na vijiji 24 kwa kufanya mikutano ya ndani na hadhara," amesema Okash.


Mgombea huyo ambaye baadhi ya viongozi na wananchi wanamwita mama mpambanaji, jasiri na shupavu amekuwa anaomba kura kwa kada mbalimbali katika jamii wakiwemo mama lishe, wajasiriamali, wamachinga, waendesha bodaboda na bajaji, vijiwe vya kahawa, saluni, sokoni, stendi na hata kwenye vilabu vya pombe.


Kila Kata na vijiji anavyokwenda, Okash amekuwa akifanya kampeni kwa ustaraabu na umakini mkubwa kiasi cha kuwajengea hamasa wananchi ya kukubali kuwapigia kura wagombea wa CCM siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28.


Okash, kila anapokwenda kufanya kampeni amekuwa akisifiwa kwa mtindo wake wa kuomba kura kwa unyenyekevu akiwa amepiga magoti lakini pia kwa mpangilio wake mzuri wa maneno yenye mvuto na ushawishi mkubwa kiasi cha kila mara kupigiwa makofi.


Amekuwa akiutumia muda wake mwingi kuomba kura za Mgombea Urais kupitia chama hicho, Dk. Magufuli kwa kuelezea sera nzuri za chama na mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na mambo mazuri yaliyomo kwenye Ilani ya CCM yanayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.


Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), wilaya ya Kongwa, Alpha Mwegalawa  aliyeambatana na Okash kwenye kampeni katika baadhi ya vijiji katika Kata za Chamkoroma na Iduo, anasema ndani ya siku tatu alikuwa naye amefanya mambo makumbwa, ameutumia muda wake mwingi kujikita kumuombea Dk Magufuli kura.


"Amefanya kampeni kiukweli ukweli, huyu mama ameiva kisiasa, ndani ya siku tatu amejitolea muda wake kisawasawa kumuombea kura Dk. Magufuli, akiwa jukwaani anaeleweka kwani anapangilia vizuri maneno, yaani hata akiongea sura yake inaonesha dhahiri anaomba kura si mzaha, Mungu ambariki afike mbali kisiasa," alimazia kusema Mwegalawa.


Amekuwa akiwakumbusha mambo makubwa yaliyofanywa katika kipindi cha miaka mitano cha Dk.Magufuli kwa mkoa wa Dodoma kuwa ni;Dodoma kutangazwa kuwa Jiji, kuwa makao makuu ya nchi, Rais kuhamia Ikulu ya Chamwino, serikali nzima kuhamia, Ujenzi wa Stendi ya Kisasa na Soko la Kisasa la Job Ndugai.


Miradi mingine ni;Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR Dar- Dodoma, kuanza kwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato na kuanza ujenzi wa barabara za pete (Ringroads) kulizunguka jiji la Dodoma na hivi karibuni JPM ametangaza kujenga Uwanja Mkubwa wa Kisasa wa michezo.


Hivi karibuni Okash alifanya tukio la kijasiri aliwahamasisha wanawake wa Kata ya Nhinhi, Jimbo la Mvumi, Dodoma, kwa kuwaongoza kwenda kwenye vilabu vya pombe kuomba kura za Dk. Magufuli na wagombea wengine wa CCM. Anasema kilichomsukuma kuchukua uamuzi huo ni baada ya kuona asilimia kubwa ya wanaume hawahudhurii mikutano ya kampeni.


Akielezea kuhusu tukio hilo la kushtukiza, Mzee Mathayo Mazengo mmoja wa wanywaji, alisema kuwa kwanza walistuka kuona kundi la wanawake wakiwemo pia wake zao wakiwaendea eneo walilokuwa wakistarehe, lakini baada ya Okash kuwaelezea lengo lao na kuwaomba kura kistaraabu walifurahi na kukubaliana naye.


Mazengo anasema, huyo binti (Okash), ni jasiri na mpambanaji mzuri, tena ana lugha nzuri ya ushawishi kiasi kwamba hata mpinzani ni rahisi kukubaliana naye.


Tukio lingine alilolifanya ni yeye kuambatana na viongozi wengine wa CCM kwenda kuzitafuta kura kwa Mama Lishe, Saluni za kike na kiume pamoja na vijiwe vya kahawa katika mitaa mbalimbali ya Jimbo la Chemba.


Pamoja na kuwaombea kura wagombea wa CCM, lakini vilevile waliunga mkono biashara zao kwa kununua vyakula na kunywa kahawa huku wakimwaga sera pamoja na kuelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk Magufuli.


Walipita katika Kata mbalimbali za Chemba ikiwemo Kata ya Msaada, ambapo walikutana na watu wa kada tofauti, wakiwemo wazee, vijana, wanawake, Mama Lishe na wauza kahawa.


Wengi wa waliowatembelea na kuwaeleza mafanikio ya Serikali ya CCM inayoongozwa na Dk. Magufuli, walifurahi kuwaona viongozi hao na kufarijika kwa kuthaminiwa, hivyo kuahidi kumpigia kura Dk Magufuli, wabunge na madiwani wa CCM katika uchaguzi utakaofanyika Jumatano ijayo Oktoba 28.


Mwishoni mw wiki, Okash alifanya kampeni za nguvu kwa kwa kugawa picha za Mgombea Urais wa CCM, Dk. Magufuli katika Stendi Kuu ya Mabasi ya Dodoma na Soko Kuu la Job Ndugai. Alizigawa kwa mawakala wa uuzaji tiketi,  vibanda vya biashara, migahawani, madareva wa mabasi na makondakta, waendesha bodaboda na bajaji, kwenye daladala na abiria waliokuwa wakisubiri usafiri.


Hivi sasa anaendelea na kampeni  katika kata mbalimbali za Jimbo la Bahi ambapo pia anatoa elimu ya jinsi ya kupiga kura Oktoba 28.


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana