Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari Hispania ikiwemo jarida Mundo Deportivo inaripotiwa Rais wa FC Barcelona Josep Maria Bartomeu ameandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo.
Bartomeu inaarifiwa ameamua kufikia maamuzi hayo baada ya wajumbe wa bodi kujiuzulu huku yeye akikumbwa na shinikizo la kutakiwa ajiuzulu na mashabiki na wanachama wa club hiyo kuonesha kukosa imani nae.
Hata hivyo Bartomeu ambaye baadhi ya watu wanaamini kuwa amejiuzulu kama sehemu ya kupisha kipenzi cha Barcelona Lionel Messi aendelee kuwepo, kabla ya dirisha la Usajili kufungwa aliripotiwa kuwa alisema kama Messi anataka kuondoka Barcelona kwa sababu yake basi atajiuzulu.
Post a Comment