Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, TAWA, Imani Nkuwi Akizungumza na Rais mstaafu kutoka The safari club international ya nchini Marekani, Steve skold.
Meneja wa Pori la Akiba la Moyowosi, Bigiramungu Kagoma akizungumzia kuimarika kwa mazingira ya pori hilo
****************************** ****************************** *
MAMLAKA ya usimamizi ya wanyamapori Tanzania TAWA na Rais mstaafu wa Klabu kubwa ya uwindaji wa kitalii duniani Steve Skold wamekubaliana kushirikiana katika kuitangaza Tanzania kuwa eneo bora la uwindaji wa kitalii.
Hayo yamebainika mara baada ya Naibu Kamishna wa Uhifadhi Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA, Imani Nkuwi kukutana na kufanya mazungumzo na Rais huyo mstaafu kutoka The safari club international ya nchini Marekani, Steve skold.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika pori la Akiba la Moyowosi lilopo Wilaya ya Kibondo, Mkoani Kigoma ambapo Rais huyo mstaafu amekuja kufanya uwindaji wa kitalii mara baada ya kumaliza kipindi chake cha uongozi mwaka 2019 akiwa ameambatana na muwindaji maarufu wa kitalii.
Klabu hiyo kubwa duniani ina wanachama zaidi ya 50,000 na matawi 200 ndani ya Marekani na 106 nje ya Marekani.
Mazungumzo hayo yamelenga kutumia fursa ya ujio wa Rais Mstaafu wa Safari Club International kutangaza utalii wa uwindaji nchini.
Aidha, Steve alifanya mahojiano maalum baadhi ya vyombo vya habari nchini ambayo na kueleza kuwa Tanzania ni sehemu bora ya kufanya uwindaji wa kitalii katika mazingira halisi ( natural habitat) yenye bioanuai nyingi za maua, wadudu na ndege wengi na wazuri.
Safar Club International Kila januari hadi februari ya kila mwaka huandaa maonesho makubwa ya uwindaji duniani ambayo yanahudhuriwa na waoneshaji zaidi ya 650,000 hivyo ni fursa nzuri kwa nchi ya Tanzania kuzidi kutangaza utalii huo wa kiwindaji.
Kwa upande wake Naibu kamishna Nkuwi alisema nchi ya Marekani kwa zaidi ya miaka 10 imekuwa iliongoza kwa asilimia 65 hadi 70 kwa wananchi wake kufanya utalii wa uwindaji nchini na hivyo ndio soko kubwa la aina hiyo ya utalii.
Aidha amesema fursa hiyo muhimu ya kushirikiana na bwana Steve katika kuwashawishi wamarekani kuwekeza katika kampuni za kuendesha utalii wa uwindaji ( hunting outfitters) na kuwaleta wamarekani wengi zaidi.
Pia Naibu Kamishna wa Uhifadhi Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA, Imani Nkuwi ameitaka jamii kujiepusha na vitendo kijangili jambo ambalo litaisaidia kupata maendeleo.
Nae meneja wa Pori la Akiba la Moyowosi, Bigiramungu Kagoma amesema kuwa mazingira ya pori hilo yanazidi kuimarika,
Bigiramungu ameongeza kuwa eneo hilo ni muhimu pia katika uwindaji hivyo kuwataka wananchi kuhakisha wanahifadhi rasiliamli hiyo muhimu kwa maendeleo yao.
Mmoja wa wawekeza katika Pori hilo, Adam Clements amesema kuwa hivi sasa wanampango wa kuisaidia jamii inayoishi pembezoni mwa kitalu hicho katika sekta ya elimu,ikiwemo kujenga madarasa,pamoja na madawati ili iweze kujiepusha na vitendo vya kijangili.
Adam amesema kuwa wanaamini kwa kufanya hivyo jamii inayozunguka eneo hilo watajua umuhimu wa uwindaji wa kitalii,pamoja na faida za wanyamapori katika maeneo yao
Post a Comment