Featured

    Featured Posts

YANGA YATAKATA YAIPIGA POLISI 1-0

 Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

KOCHA mpya, Mrundi Cedric Kaze ameanza na ushindi mwembamba wa Yanga SC baada ya kuiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza leo na kuichapa 1-0 Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Pongezi zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee kipindi cha pili.
kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mukoko Tonombe ambaye hapa Tanzania amepewa jina la utani Teacher, yaani Teacher kutokana na staili yake ya ushangiliaji.

Tonombo aliye katika msimu wake wa kwanza tu tangu asajiliwe kutoka AS Vita ya nyumbani kwao, Kinshasa amefunga bao hilo dakika ya 70 kwa shuti lilombabatiza beki wa Polisi Tanzania baada ya kupokea pasi ya kiungo Mzanzibari, Feisal Salum.




Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, wenyeji Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Simba SC bao pekee la Samson Mbaraka Mbangula dakika ya 49 akimalizia kazi nzuri ya Michael Ismail Mpesa Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa. 

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Mukoko Tonombe, Tusila Kisinda, Feisal Salum, Yacouba Sogne/Michael Sarpong dk62, Haruna Niyonzima/Ditram Nchimbi dk59 na Farid Mussa/Zawadi Mauya dk77.
Polisi Tanzania; Peter Manyika, Datius Peter, Juma Hajji, Iddy Mobby, Mohammed Kassim, Pato Ngonyani, Rashid Juma/Hamad Kambangwa dk56, Hassan Maulid, Tariq Seif, Marcel Kaheza/Kassim Haruna dk77 na Pius Buswita. 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana