Wazanzibari leo wanapiga kura ya mapema ambapo makundi maalum wakiwemo Watumishi wa Tume ya Uchaguzi (ZEC) na Wasimamizi wa Uchaguzi watashiriki katika zoezi hilo.
Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Hamid Mahmoud Hamid amesema wanaopiga kura leo watatumia Vituo ambavyo wamejiandikisha, kura zao zitahifadhiwa na kulindwa ili kujumlishwa na kura zitakazopigwa kesho.
Aidha, amesema Vyombo vya Ulinzi pia vitapata nafasi ya kupiga kura leo huku akisisitiza sio Askari wote watakaoshiriki bali ni wale watakaohusika kusimamia shughuli za Uchaguzi
.
Post a Comment