Featured

    Featured Posts

CHADEMA YAWAVUA UANACHAMA WABUNGE 19 WALIOAPISHWA

 

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema Kamati Kuu ya Chama hicho iliyoketi  Nov 27,2020 imeazimia kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 waliopishwa kuwa Wabunge Viti Maalum “wamekinajisi Chama na wamekataa kuja kwenye Kamati Kuu”

”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaapishwa” Mbowe

“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka” Mbowe 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana