Featured

    Featured Posts

DK. MAGUFULI, DK. SHEIN NA WAGENI KUTOKA NCHI ZA NJE IKIWEMO CHINA KUNOGESHA KUAPISHWA DK. HUSSEIN MWINYI KESHO


Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar DK. Abdulah Juma Sadala, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui mjini Unguja, leo.
 
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

Rais Mteule wa Tanzania ambaye ni Rais anayemaliza mhula wake wa kwanza wa Urais Dk. John Magufuli na Rais wa Zanzibar anayemaliza muda wake Dk. Ali Mohamed Sheni na Wageni mbalimbali kutoka nchi za kadhaa zikiwemo Namibia, Msumbiji, Uganda, Ghana, Kenya, China, Moroco, DRC Kongo, pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa wanatarajiwa kunogesha  hafla ya kuapishwa Rais mteule wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi katika  Uwanja wa Amani Abeid Karume mjini Unguja.


Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui mjini Unguja, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar DK. Abdulah Juma Sadala alisema mabalozi zaidi ya 26 wa ndani na  nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki katika ghafla hiyo.


Alisema, wageni wengine wanaotarajiwa kushiriki katika sherehe hizo ni pamoja na vyama rafiki vya siasa kutona nchi mbali mbali kama vile, Namibia, Msumbiji, Uganda, Ghana, Kenya, China, Moroco, DRC Kongo, pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa.


Hata hivyo DK. Mabodi aliwataka wananchi mbali mbali wa Zanzibar na nje ya Zanzibar kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Amani kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa awamu ya nane wa Zanzibar.


"Nakuombeni sana mje kwa wingi wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi mje kushuhudia kile ambacho mlikiamua katika chumba cha kupigia kura Oktoba 28," alisema.


Aidha aliwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kuweza kumpa ushindi wa kishindo mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi DK. Hussein Ali Mwinyi na kufanya apate ushindi wa asilimia 76 ushindi ambao ni wa kihistoria.


Alisema, wananchi wa Zanzibar wameonyesha kwa kiasi kikubwa imani yao juu ya Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi wa mwaka huu na kuahidi kuwa Chama hicho kitashirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo ya nchi.


Aidha aliwashukuru pia wananchi hao wa Zanzibar kwa kuwachagua kwa wingi Wabunge, Wawakilishi na Madiwani wa Chama cha Mapinduzi na kukifanya Chama hicho kuchukua jumla ya Majimbo 45 kati ya Majimbo 50 yaliyopo Unguja na Pemba.


Akizungumzia siri ya ushindi wa CCM, alisema ni uwepo wa sera imara,kampeni za kisayansi za kuwafuata wananchi katika makaazi yao kuwaeleza namna watakavyotatuliwa changamoto zao sambamba na utekelezaji mzuri wa ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020.

 

Alisema CCM imeendelea kuwa muumini mkubwa wa kulinda amani na utulivu nchini ili wananchi wapate uhuru wa kufanya shughuli zao za maendeleo kwa utulivu.


MAANDALIZI YA UWANJA


Maandalizi ya uwanja wa kuapishwa kwa Rais Mteule huyo yamekamilika kwa kiwango kikubwa katika Uwanja wa Amani Abeid Karume.


Mwandishi wa gazeti hili jana alifika katika viwanja hivyo na kukuta taratibu za mwisho za maandalizi ya viwanja hivyo zikiendelea.


Viwanja hivyo vya Amani vimepambwa kwa rangi za bendera ya Tanzania Blu, Nyeusi, Kijani na Njano pamoja na rangi za bendera ya Zanzibar


Lakini pia katikati ya viwanja hivyo kumeandaliwa jukwaa maalum ambalo ndiyo itakuwa sehemu ya kuapishwa kwa Rais mteule huyo wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 


Milango ya kuingia kwenye viwanja hivyo itafunguliwa majira ya saa 12:00 asubuhi ili kutoa fursa kwa wananchi kuwahi kufika viwanjani hapo na kushudia tukio hilo adhimu ambalo hupatikana kila baada ya miaka mitano.


Akingumza katika shughuli ya maandalizi ya uwanja huo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Hassan Khatibu Hassan alisema, maandalizi yote yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika shughuli hiyo muhimu kwa taifa. 


Alisema wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na wa mikoa mengine wasiwe na wasiwasi kuhusu usalama wao kwani suala la ulinzi na usalama limeimarishwa kwa kiwango kikubwa.  


Hata hivyo alisema, wanachi wengine kutoka kisiwa cha Pemba nao watashiriki shughuli hiyo muhimu ya kuapishwa kwa Rais Mteule wa Zanzibar


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya habari Maalezo zanzibar DK.Juma Mohammed aliwataka wananchi wajitokeze mapema ili kuondosha usumbufu wa kuchelewa kuingia katika uwanja huo. 


CAPTIONS


DSC - 0210,0231- NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi,akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya sherehe za kumuapisha Rais mteuli wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana