Featured

    Featured Posts

DK MAGUFULI KUAPISHWA ALHAMISI NOVEMBA 5


 Na Richard Mwaikenda, Dodoma.

RAIS Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. John Magufuli ambaye leo amekabidhiwa na NEC cheti cha uchindi, anatarajiwa kuapishwa kushika rasmi wadhifa huo katika sherehe zitakazofanyika Alhamis Novemba 5 kwenye Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Dk Magufuli ambaye aligombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi,CCM, ameshinda ushindi wa kimbunga kwa kupata zaidi ya kura milioni 12 ambazo ni sawa na zaidi ya asilimia 84.


Katika sherehe hizo pia ataapishwa aliyekuwa Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Mteule wa Zanzibar aliyegombea kupitia CCM, Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuapishwa kesho Unguja Zanzibar.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana