Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF), Ahmad amepigwa marufuku ya miaka mitano na Shirikisho la soka duniani Fifa kwa kukiuka sheria kadhaa za maadili.
Makamu huyo wa rais wa Fifa mwenye umri wa miaka 60 amedaiwa kukiuka sheria ya maadili inayohusisha jukumu lake la utiifu, kwa kutoa na kupokea zawadi hatua ambayo ni kinyume na wadhfa wake mbali na utumizi mbaya wa fedha.
Uchunguzi kuhusu tabia ya Ahmad kutoka mwaka 2017 hadi 2019 ulihusu masuala ya utawala wake katika Shirikisho hilo pamoja na kuandaa na kufadhili safari ya kuhiji Mecca ya Umrah, kuhusishwa kwake katika kashfa ya kampuni ya vifaa vya michezo ya Tactical Steel na shughuli nyengine , ilisema taarifa ya Fifa.
Ahmad pia amepigwa faini ya dola za Marekani 200,000
.
Post a Comment