CCM Blog, Dodoma
Sitaki nataka' ya Chadema hatimaye imeishia ukingoni baada ya Wabunge wake 19 wa Viti Maalum Chadema kuapishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai katika Viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.
Baadhi ya walioapishwa ni aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chadema lakini akashindwa vibaya na Mbunge wa sasa katika jimbo hilo kwa tiketi ya CCM Askofu Josephat Gwajima, katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu.
Mbali na Halima Mdee ambaye amelazimika kurejea Bungeni kupitia kapu hilo la viti maalum, ni Grace Tendega, Esther Matiko, Jesca Kishoa na Ester Bulaya.
Endelea kufuatilia Blog hii ya Taifa ya CCM kwa taarifa zitakazojiri zaidi.
Post a Comment