Naibu Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bw. Ephraim Mwangomo (Kushoto) akikabidhi zawadi ya tisheti na Miamvuli kwa Viongozi wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa Miaka 20 mara baada ya timu hiyo kupata Ushindi mnono wa goli 8-1 dhidi ya timu ya Somalia katika Mashindano ya CECAFA yanayoendelea Wilayani karatu Mkoani Arusha, Kulia ni Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi (Huduma za Utalii) Bw. Paul Fissoo.
Timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa Miaka 20 wakiwa katika geti kuu la Kuingilia Hifadhi ya Ngorongoro (Loduare Gate) mara baada ya kuhitimisha mchezo wao na timu ya Taifa ya Somalia.
Timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa Miaka 20 wakiwa katika eneo la View point ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro baada ya timu hiyo kutoka kufanya mazoezi katika viwanja vya makao vilivyopo mkabala na ofisi za Makao makuu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Matukio mbalimbali wakati wa mchezo kati ya timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa Miaka 20 na timu ya Vijana ya Somalia, katika Mchezo huo timu ya taifa ya Vijana iliichapa timu ya Vijana ya Somalia kwa jumla ya magoli 8-1
Post a Comment