Rais Dk. John Magufuli amewateua Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole na Riziki Said Lulida kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Chamwino jijini Dodoma, Gerson Msigwa imesema, Wabunge hao wateule wataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Post a Comment