Ikulu, Chamwino.
Rais Dk. John Magufuli amewateua Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Ali Mohammedhein, Waziri Mstaafu wa Habari, Sanaa Utamadini na Michezo Dk. Harison Mwambe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudentia Kabaka kushika nyafidha mbalimbali za uongozi.
Taarifa iliyosambazwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, leo baada ya kutolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imisema Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Shein, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe kuchukua nafasi ya Jaji Mstaafu Barnabas Samatta ambaye anamaliza muda wake.
Imesema, Dk. Mwakyembe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kuchukua nafasi ya Mariam Mwaffisi ambaye pia amemaliza muda wake, Gaudentia Kabaka akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ikiwa ameteuliwa kushika nafasi kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika. Taarifa hiyo imesema kuwa uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 24 Novemba, 2020.
Post a Comment