Featured

    Featured Posts

SHILINGI MILIONI 270 ZA MISITU ZALETA MAPINDUZI NANDENJE

 

NA SULEIMAN MSUYA, RUANGWA
KIJIJI cha Nandenje, Kata ya Mandarawe, Wilayani Raangwa mkoani Lindi, kimetumia zaidi ya shilingi milioni 279  zilizokusanywa kupitia dhana ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (USMJ), kutekeleza miradi ya kijamii na maendeleo.
Dhana ya USMJ kijijini hapo imefikishwa na Shirika la  Kuhifadhi Mpingo na Maendeleo (MCDI) kupitia Program ya Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu (FORVAC), inayotekelezwa n Idara ya Misitu na Nyuki chini ya Serikali ya Tanzania na Finland.
Program ya FORVAC inatelelezwa katika kongano tatu ambazo ni Tanga yenye wilaya za Handeni, Kilindi, Mpwapwa na Kiteto, Ruvuma ni wilaya za Tunduru, Nyasa, Mbinga na Songea na Lindi ni Ruangwa, Liwale na Nachingwea.
Kwa mujibu wa Mtendaji wa Kijiji cha Nandenje Rashid Kajete amesema fedha hizo zimekusamywa kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 baada ya wanakijiji kupatiwa elimu na kutambua umuhimu wa USMJ kwenye vjjiji vyao.
Awali kijiji hakikuwa na uelewa kuhusu USMJ ila kila mtu ni mlinzi wa msitu kwani faida inaonekana.
Mtendaji amesema fedha hizo zimefanikisha ujenzi wa Zahanati ya Nandenje kwa zaidi ya shilingi milioni 49, nyumba ya mganga shilingi milioni 36, choo cha zahanati shilingi milioni 4.3, kichomea taka shilingi milioni 8 na kununua maeneo yanayozunguka zahanati kwa shilingi milioni 1.6.
“Ujenzi wa nyumba walimu shilingi milioni 39, ukarabati nyumba za walimu shilingi milioni 2, Shule ya Sekondari Mandarawe shilingi milioni 40, ununuzi wa eneo la kujenga shule shilingi milioni 3.8,” amesema Kajete.
Amesema fedha hizo zimetumika  kununua trekta shilingi milioni 67.8, ujenzi wa jengo ka kuhifadhia trekta shilingi milioni 3.7 pamoja na ununuzi wa eneo la soko kwa shilingi 700,000.
Amesema mafanikio hayo yametokana  na utekelezaji wa sera ya misitu ya mwaka 1998 inayotoa kipaumbele kwa jamii kushirikishwa katika usimamizi wa wa misitu kwa lengo kukuza kipato cha jamii ili kupunguza umaskini.

Amesema kupitia USMJ wanakijiji wekuwa na amani na upendo kwa kuwa hawabughudhiwi kwa kuombwa michango bali wanakaa kujadili matumizi ya fedha zinatokana na uvunaji endelevu wa misitu.

“Katika kipindi hicho Halmashauri ya Ruangwa imekusanya zaidi ya shilingi milioni 47.9 ambapo kamati ya misitu ya kijiji imekusanya zaidi ya  shilingi milioni 153 ni mafanikio makubwa.
Mtendaji amesema kijiji kina watu wapatao 2,200 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 na  ukubwa wa hekta 12,745.48 na kwamba hekta 5025 ni hifadhi ya misitu ndio inachochea maendeleo hayo makubwa.

Kajete ameongezea kuwa kijiji kina mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya kilimo, ufugaji na makazi ya watu  hali ambayo imepunguza migogoro baina yao.

Mtendaji amesema shilingi milioni 279 zepatikana baada ya kununwa miti michache ambayo ni Msekeseke, Mninga, Mtondolo, Mnangu na Mkongo huku misitu ukiwa salama.

Mjumbe wa Serikali ya kijiji hicho Juma Rashid amesema USMJ umeweza kuwakombo kiuchumi, kijamii na maendeleo hivyo watahakikisha misitu inakuwa salama.

Rashid amesema kupitia miradi hiyo kuanzia mwakani watoto wao watatembea umbali mdogo kwenda shule hivyo ufaulu utaongezeka na mimba za utotoni zitapungua kama sio kuisha kabisa.
“Hayo aliyosema mtendaji ni ya kweli na sababu ya yote hayo ni misitu yetu ambayo tunaitunza kwa uendelevu,” amesema.
Kwa upande wake Salima Alli amesema kwa sasa ana amani kwani misitu imesaidi kuwepo n jinsia kijijiji kwao kwa wanawake wengi kushiriki kwenye maamuzi jambo ambalo awali halikuwepo.
Amesema kamati mbalimbali za kijiji zina wanawake ila ujasiri na usubutu umetokana na ushiriki wao kwenye USMJ.
Ofisa Misitu wa Wilaya ya Ruangwa James Kabuta amesema halmashauri hiyo inachukua asilimia 10 ya mapato yote ya mazao ya misitu kutoka kwenye Kijiji ambapo asilimia 60 inakwenda kijijini na asilimia 30 kamati ya misitu ya kijiji.

Amesema  halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa uhifadhi ikiwemo FORVAC, MCDI, WWF, MJUMITA, CoFOREST na wengine wanaelekeza nguvu kubwa kwenye elimu kwani ndio mkombozi katika dhana ya. USMJ.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ruangwa, Mohamed Muhidin amesema halmashauri itashirikiana na mdau yoyote ambayo atakuja na dhana inayowezesha misitu kuwa endelevu kwa kuwa faida wanaiona kwenye vijiji vya miradi kati ya vijiji zaidi ya 90 walivyo navyo.
Msimamizi na Mtaalamu wa Misitu wa Program ya FORVAC,Alex Njahani amesema mradi huo umegusa maisha ya watu zaidi ya 330,000 hivyo ni wazi kuwa ni mzuri kiuhufadhi, kiuchumi na maendeleo.
Njahani amesema lengo la program ni kuona kila mwanajamii anayezungukwa na misitu ya jamii wananufaika na uhifadhi unaendelea.
“Tumenunua  mashine za kisasa za kuchakata mbao inayotembea (Mobile Sawmill) kwa ajili ya mkoa wa Lindi na Ruvuma ambapo uzalishaji umeongezeka zaidi,” amesema.
Njahani amewashauri wanavijiji kulinda na kuhifadhi misitu ili iwe endelevu kwa vizazi vya sasa na baadae.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana