Uongozi wa Mkoa wa Tabora umekutana na wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi na saruji na kukubaliana faida wanayopata katika kila mfuko mmoja wanaouza isizidi Sh 500 ili kutowaumiza wananchi wanyonge.
Wamefikia uamuzi huo katika mkutano ambao uliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk. Philemon Sengati, kwa lengo la kutafuta muafaka wa kutatua tatizo la bei ya saruji kupanda.
Dk. Sengati amesema Serikali haikusudii kuwapangia bei elekezi ya saruji lakini wafanyabiashara wanalo jukumu la kuuza bidhaa hiyo kwa bei ambayo haitawafanya wananchi wanyonge washindwe kujenga na kuishi katika nyumba bora.
Dk. Sengati amesema kimsingi hakuna sababu zinazoweza kuhalalisha wafanyabiashara hao kupandisha saruji ambapo wapo wanaouza Sh 23,000 hadi 30,000 kwa mfuko mmoja wakati wao wananunua kiwandani kwa wastani unaoanzia Sh 11,000 hadi 13,00
0
Post a Comment