Zinafanyika harakati za kuunda Jukwaa la wanaume ili wale wenye dukuduku zinazoweza kuwaletea hatari ya kupatwa na usongo wa mawazo na hatimaye kujidhuru, waweze kuzisema kwenye jukwaa hilo ili wapumue na kuondokana na hatari hiyo ya kuweza kujidhuru.
Hayo yamesemwa kwemye Kongamano la Wanaume lililofanyika jijini Arusha Disemba 12, 2020 katika ukumbi wa Cloud View Mtaa wa Sakina kwa lengo la kujadili na kupata ufumbuzi wa matatizo ya Wanaume yatokanayo na wanaume kujidhuru kutokana na msongo wa mawazo unaosababishwa na kukabiliwa na mambo mbalimbali yakiwemo ya kifamilia na kimaisha kwa jumla.
Katika kongamano hilo imeelezwa kuwa kuna iIdadi kadhaa ya Wanaume wanaokufa kutokana na msongo wa mawazo inayoongezeka ambapo idadi ya Wanaume hufikwa na vifo kutokana na kukumbwa na shambulio la moyo, kujinyonga na kutolewa mfano kuwa hivi karibuni tkuna matukio mawili jijini Arusha la mmoja kufa ghafla na mwingine kujinyonga ikiwa ni ushahidi tosha wa jambo hilo kuzidi kushamiri.
"Tumeamua tujadili na tuwahamasishe Wanaume kuondoa ukimwa Ili tuanze kuongea mambo yanayotusumbua na hii itasaidia kupunguza kwa matendo ya kujiadhuru na hata kupunguza ukatili ambao unatokana na mlimbikizo wa hasira", amesema Evance Chipindi ambaye ni mmoja wa waandaaji wa Kongamano hilo akishirikiana na Mwezeshaji mwezake Waziri Njau, ambao wote ni wataalam wa masuala ya Kunufaisha jamii kwa njia za vikundi vya Usasiriamali na Vikoba hasa kwa kina mama.
"Mambo mengi yamejadiliwa na maazimio mbalimbali yametolewa Ili jambo hili liwe endelevu na hatimaye liundwe jukwaa kamili la Wanaume ambapo watapata nafasi ya kujadili mambo yawahusuyo kwa uwa miongoni mwa sababu zinazofanya wanaume kujidhuru ni kukosa nafasi ya kuyaeleza kwa wengine mazonge yanayowakabili ili waweze kusaidiwa njia za kuyatatua au kuyavimilia", amesema Chipindi na kuongeza;-
"Kongamano hili lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka mabenki, mashirika ya kijamii, vyuo vikuu, boda boda, madereva teksi, wachungaji, waandishi wa habari na wawakilishi wa vikundi vya VICOBA jijinia Arusha na miongoni mwa maazimio ni pamoja na 1. Kuundwa kwa jukwaa la kudumu ambalo wadau tutakutana kila miezi mitatu, 2. Kutoa elimu itakayo wawezesha Wanaume kuendelea kuongea badala ya kukaa na mambo moyoni
3. Wanaume kuacha kufanya maamuzi ya haraka kwa mfano tabia za kugawana mali watu wanapo achana na matokeo yake mali hizo kuuzwa kwa gharama ndogo kama njia ya kukomoana na 4. Wanaume kuonyesha upendo na kujali pale inapobidi na pale mambo yanapokuwa magumu basi wadau tunashirikishwa na kutolea ufumbuzi".
Chipindi amesema Kongamano hilo limefanyika kwa ufadhili wa Taasisi ya UTT Ami's inayojishughulisha na Uhamasishaji wa uwekaji wa fedha na akiba kwa mwananchi kwa matumizi ya baadaye, taasisi hiyi makao yake yapo jijini Arusha katika Jengo la Ngorongoro
Post a Comment