Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mhe. Harold Nsekela amefariki dunia asubuhi, Desemba 06, 2020 mjini Dodoma baada ya kuugua kwa muda Mfupi.
Taarifa Zaidi kufuatia Msiba huo pamoja na taratibu nyingine za mazishi zitajulikana baadaye. Marehemu Jaji Mstaafu Nsekela alizaliwa Oktoba 21 mwaka 1944.
Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa twitter ameandika “Nimesikitishwa na kifo cha Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Harold Nsekela. Poleni familia, watumishi wote wa Sekretarieti ya Maadili na Mahakama. Jaji Mstaafu Nsekela alikuwa mwadilifu, mzalendo, asiyejikweza na mchapakazi. Mungu amweke mahali pema”
.
Post a Comment