Kocha wa Plateau United ya Nigeria baada ya kuondolewa na Simba SC katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika amelia na hujuma anazodai walitaka kufanyiwa toka wamewasili Airport DSM.
“Toka tulipowasili Airport tulitishiwa kwa sababu walitaka kuwaondoa baadhi ya wachezaji wetu wasicheze hii mechi (Waseme wana Corona) tukiwa na wachezaji hawa hawa walishinda Nigeria kwa nini waogope”>>>> Abdul Maikaba
Platea United walitolewa na Simba SC kwa aggregate ya goli 1-0 ambalo walifungwa Novemba 29 2020 wakiwa nyumbani kwao Jos Nigeria, hivyo kwa kuwa mchezo wa December 5 wa marudiano kwa mkapa wameshindwa kufungana na kuishia 0-0 basi Platea wanaaga michuano hiyo na Simba sasa itacheza dhidi ya FC Platnum ya Zimbabwe mjini Harare Decemba 22-23 na marudiano January 5-6 2021 Dar es Salaam
.
Post a Comment