Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Musumbiji Bernadino Rafael amesema magaidi katika Mkoa wa Cabo Delgado, Kaskazini mwa nchi hiyo wanakufa kila siku kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo njaa, kutokana na jeshi hilo kukata mfumo wao wa ugavi.
Amesema, vikosi vya ulinzi na usalama vimefanikiwa kuwazuia magaidi hao kufika katika mikoa mingine ikiwemo Maputo.
Pia ameeza kuwa bado hajui idadi halisi ya wapiganaji katika kikundi cha ugaidi kwa kuwa kila siku magaidi wanaandikisha watu wapya, na kwa upande mwingine wengi wao wameuawa katika mapigano na vikosi vya ulinzi na usalama.
Post a Comment