Ikulu, Chamwino.
Rais Dk. John Magufuli leo tarehe 05 Disemba, 2020 amekamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo, Rais Magufuli amewateua Mawaziri 21 wakiemo wawili abao amewateua pia kuwa wabunge. Mawaziri hao wataungana wale Mawaziri wawili walioteuliwa tarehe 13 Novemba, 2020. Pia Rais amewateua Naibu Mawaziri 23, huku Rais akiongeza Wizara moja mpya ambayo ni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Mawaziri ambao Rais Rais Magufuli alishawateua na kuwaapisha ni;
Dk. Philip Isdor Mpango – Waziri wa Fedha na Mipango na Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi – Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.Mawaziri wapya ni kama ifuatavyo;👇
Naibu Mawaziri walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
1. Kigahe Exaud Silaoneka kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara. 2. Dk. Angelina Sylvester Lubala Mabula kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. 3. Patrobas Paschal Katambi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira). 4. Khamis Hamza Khamis kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. 5. Mwanaidi Ali Khamis kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango. 6. Kipanga Juma Omary kuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia. 7. Dkt. Festo Stephen Dugange kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI). 8. Byabato Stephen Lujwahuka kuwa Naibu Waziri wa Nishati. 9. John Deogratius Ndejembi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora). 10. Mhandisi Kundo Andrea Mathew kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. 11. Pauline Philipo Gekul kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi. 12. Ndulane Francis Kumba kuwa Naibu Waziri wa Madini. 13. Msongwe Godfrey Kasekenya kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi. 14. Ummy Hamis Nderinanga kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu).15. Mhandisi Marryprisca Winfred Mahundi kuwa Naibu Waziri wa Maji.
16. Abdallah Hamis Ulega kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. 17. Mwita Mwikwabe Waitara kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). 18. William Tate Ole Nasha kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 19. Marry Francis Masanja kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii. 20. David Ernest Silinde kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI). 21. Hussein Mohamed Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo. 22. Dk. Godwin Oloyce Mollel kuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. 23. Geophrey Mizengo Pinda kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.Wateule wote wataapishwa wiki ijayo Jijini Dodoma kwa tarehe na muda utakaotangazwa baadaye.
Post a Comment