Featured

    Featured Posts

MWANAHAARI ALIYEIBUA HABARI YA MLIPUKO WA CORONA CHINA AFUNGWA JELA


Mwanahabari wa China amefungwa jela miaka minne kwa kuripoti kutokea Wuhan wakati mlipuko wa Covid-19 ulipoanza, ikiwa ni mwaka mmoja baada ya maelezo kuhusu kirusi kisichojulikana cha nimonia kujitokeza katika mji huo wa katikati mwa China.

Zhang Zhan ambaye ni wakili wa zamani, amehukumiwa katika mahakama ya Shanghai kwa madai ya “kuchochea ugomvi” wakati akiripoti matukio ya mwanzo ya mripuko wa corona.

Ripoti zake za moja kwa moja na makala zilisambazwa kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii Februari, na kuwafikia maafisa nchini humo ambao mpaka sasa wamewaadhibu watu wanane waliofichua habari za kirusi hicho, wakati wakiendelea kupuuza ukosoaji wa serikali kuhusu namna serikali ilivyoshughulikia mripuko huo
.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana