Featured

    Featured Posts

NTIBANZONKIZA ATOKEA BENCHI NA KUFUNGA MOJA, YANGA IKIIPICHAPA DODOMA FC 3-1 ARUSHA

 

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
VIGOGO, Yanga SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Dodoma Jiji FC 3-1 jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 40 baada ya kucheza mechi 16 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nane zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi.  
Dodoma Jiji FC yenyewe iliyopanda Ligi Kuu msimu huu inabaki na pointi zake 19 baada ya kucheza mechi 14 katika nafasi ya 11.


Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mtibwa Sugar imeichapa 1-0 JKT Tanzania bao pekee la Riphat Msuya dakika ya 43 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Ihefu imeichapa 1-0 KMC bao pekee la Joseph Kinyozi dakika ya tisa Uwanja wa Highland Estates, Mbarali mkoani Mbeya.
Nayo Gwambina imelazimishwa sare ya 1-1 na Tanznaia Prisons Uwanja wa Gwambina, Misungwi, wenyeji wakitangulia kwa bao la Paul Nonga dakika ya kwanza, kabla ya wageni kusawazisha dakika ya 81 kupitia kwa Marco Mhilu. 
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwanyeto, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda, Feisal Salum, Michael Sarpong/Said Ntibanzonkiza dk46, Deus Kaseke na Yacouba Sogne/ Ditram Nchimbi dk89.
Dodoma Jiji FC; Aaron Kalambo, George Wawa, Jukumu Kibanda, Justin Omary, Mbwana Bakari ‘Kibacha’/ Rajab Seif dk73, Salmin Hoza, Dickson Ambundo, Steven Silvester/ Cleiphace Mkandala dk84, Seif Karihe, Khamis Mcha na Peter Mapunda.  
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana