Featured

    Featured Posts

RAIS WA ZANZIBAR DK HUSSEIA MWINYI MGENI AHUDHURIA TAARAB YA KUMPONGEZA KIKWAJUNI, ZANZIBARKIKWAJUNI, JANA USIKU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimia Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi.Ruth Zaipuna alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar kuhudhuria Taarab ya kumpongeza iliofanyika jana usiki 5/12/2020 na (kushoto kwa Rais) Spika wa Baraza
la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akifuatilia Taarab maalum ilioandaliwa na Benki ya NMB kwa ajil ya kumpongeza, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais) Spika wa Baraza
la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi.Ruth Zaipuna na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Maryam Mwinyi, wakifuatilia hafla hiyo ya Taarab Maalum iliofanyika jana usiku 5/12/2020
BAADHI ya Mawaziri, Viongozi wa Chama na Wananchi
wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna akitowa Salamu za NMB na kumpongeza Rais wa Zanzibar kwa ushindi wake katika uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, wakati wa hafla ya Taarab Maalum iliandaliwa na Benki ya NMB katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil
Kikwajuni Jijini Zanzibar jana usiku 5/12/2020
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akilimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna akizungumza na kutowa salamu za pongezi kwa Rais wa Zanzibar kwa ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman na (kulia kwa Rais) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Maryam Mwinyi, hafla hiyo ya Taarab rasmin iliofanyika jana usiku 5/12/2020 katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Maryam Mwinyi akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna (kushoto kwake ) na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe Asha Abdalla Juma (kulia kwake) wakienda kutunza katika hafla ya Taarab rasmin ya kumpongeza Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar jana usiku 5/12/2020.
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwaryam Mwinyi na (kushoto kwake) Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna wakijumuika katika Taarab Maalum ya kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani ) wakijumuika na Wananchi katika hafla hiyo wakati Msanii wa Kikundi cha  Zanzibar Big Star Tahir Khamis akiimba wimbo wa “ Warewarew CCM” katika hafla hiyo iliofanyika jana usku 5/12/2020 katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakiul Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha zote na Ikulu)
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana