“Hayati Shubash, ana mchango wake kwenye sekta ya viwanda, alikuwa rafiki wa wote, mcheshi, ametoa msaada kwa maskini na matajiri na hakuwa mbaguzi,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa katika Salam hizo za Rambirambi.
“Ninatoa pole kwa wanafamilia, ndugu na wote walioguswa na msiba huu. Taifa limempoteza mmoja wa wazalendo wake. Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.”
Katika salamu alizozitoa leo Desemba 15, 2020, Waziri Mkuu amesema amehuzunishwa na kifo cha mfanyabiashara huyo maarufu nchini ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI) na mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).
Mmoja wa wanafamilia amesema, Bw. Patel amefia nyumbani kwake, Kisutu jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akiendelea na matibabu na anatarajiwa kuzikwa keshokutwa (Alhamisi, Desemba 17, 2020) kwenye makaburi ya Wahindu yaliyoko Kijitonyama, Dar es Salaam.
Mfanyabiashara huyo maarufu nchini alikuwa akimiliki kampuni zinazotengeneza bidhaa za plastiki, saruji, mabati, nondo, nyaya za umeme, vinywaji, rangi na pia alimiliki hoteli za White Sands na Sea Cliff, Pearlsun Hotel & Resorts.
Post a Comment