Featured

    Featured Posts

SPIKA WA BUNGE LA DRC CONGO ANG'OLEWA

 


Muungano wa vyama vya kisiasa wa FCC wa aliyekuwa rais wa DRC Joseph Kabila umekiri kuwa kung’olewa kwa, Jeanine Mabunda kwenye wadhifa wa Spika wa Bunge la nchi hiyo ni vita kubwa na kwamba ulipoteza nafasi muhimu.

Muungano wa FCC ulioanzishwa na Kabila umetoa wito kwa wafuasi wa muungano huo kufunga vibwebwe, wakati wengi wanaendelea kujiuliza maswali kadhaa kuhusu hatma ya FCC.

Baada ya Spika Jeanine kutimuliwa mamlakani na kuvunjwa kwa ofisi ya Bunge (kuondolewa kwa wajumbe 5 kati ya 6 wa kamati kuu ya Bunge), PPRD, chama cha Kabila, hatimaye kimekiri kushindwa.

“Ushindi hauji kila wakati. Wacha tu tufikirie haraka jinsi ya kuimarisha muungano wetu. Maumivu ni makubwa, lakini tusikate tamaa. Wacha tuendelee na vita hivi, wanaharakati wapendwa,” Chama cha PPRD 

Patrick Nkanga, mmoja wa makada wa PPRD, amebainisha kuwa wakati umewadia wa kufanya mabadiliko makubwa kwa Chama cha PPRD na pia kwa Muungano wa FCC. Hii sio mara ya kwanza tunakumbwa na hali hii, huku wafuasi wengine kadhaa wa FCC wakimuunga mkono
.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana