Rais mteule wa Marekani Joe Biden atatia saini maagizo ya rais siku ya kuapishwa kwake kuwa rais wiki ijayo ili kushughulikia janga la virusi vya corona, uchumi wa nchi hiyo unaodorora, mabadiliko ya hali ya hewa na ubaguzi wa rangi.
Haya ni kwa mujibu wa mkuu wa utumishi anayetarajiwa Ron Klain.
Katika taarifa aliyoitoa jana Jumamosi, Klain amesema kuwa mizozo yote hii inahitaji kushughulikiwa kwa haraka na kuongeza kuwa Biden atatia saini takriban maagizo 12 ya rais baada ya kuapishwa siku ya Jumatano.
Klain aliongeza kuwa katika siku zake 10 za kwanza ofisini, Biden atachukua hatua madhubuti kushughulikia mizozo hiyo minne, kuzuia madhara mengine ya haraka na yasiyoweza kurekebishwa, na kurudisha nafasi ya Marekani ulimwenguni.
Post a Comment