Urusi imeuarifu Umoja wa Mataifa kwamba inawarudisha nyumbani wakufunzi 300 wa kijeshi iliyowapeleka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kusaidia kutoa mafunzo kwa jeshi la nchi hiyo.
Barua kutoka kwa ujumbe wa Urusi katika Umoja wa Mataifa kwenda kwenye kamati ya Baraza la Usalama la umoja huo inayofuatilia vikwazo dhidi ya nchi hiyo inayokumbwa na mzozo, imeeleza kuwa usaidizi wake katika uchaguzi umemalizika.
Jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati lilikuwa likikabiliwa na mashambulizi kutoka katika makundi ya waasi kabla ya uchaguzi wa mwezi uliopita.
Wakati huo huo, Urusi imetangaza kuwa inajiondoa katika makubaliano yaliyotiwa saini baada ya Vita Baridi yanayowakubalia wanachama wake kurusha ndege za kijasusi zisizo na silaha kwenye mipaka ya nchi wanachama, kwa kutoa taarifa ya muda mfupi.
Post a Comment