Baadhi ya wanachama 600 wapya wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Kitivo cha Elimu (COED), wakila kiapo cha uaminifu baada kukabidhiwa kadi na Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Umoja wa Vijana, Asia Halamga wakati wa mkutano mkuu wa UVCCM ambao uliwakaribisha pia wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo leo Januari 17,2021.
Mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), anayeshughulikia Ajira na Vijana, Patropas Katambi. Pia mkutano huo ulihudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Antony Mavunde, Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Malinyi, Antipas Mgungusi na Mbunge wa Viti Maalumu, Asia Halamga.
Vilevile katika mkutano huo alikuwepo Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Taifa, Leonard Mwakalukwa na Katibu UVCCM Mkoa wa Dodoma, Joel Makwaia.
Mwenyekiti wa UVCCM Coed Udom, ni Godfrey Masele na Katibu Mkuu ni Faris Burhan. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mbunge Asia Halamga akiwakabidhi kadi wanachama wapya wa Umoja wa Vijana Udom.
Wanachama wapya wa UVCCM wakilishwa kiapo cha uaminifu.
Baadhi ya wabunge wa CCM wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa UVCCM UDOM Coed ya Elimu
Mwenyekiti wa UVCCM Kitivo cha Elimu Coed, Godfrey Masele akiagana na Mbunge wa Hai, Saasisha Mafuwe baada ya mkutano huo kumalizika.
Post a Comment