Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Husein Bashe,akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Pembejeo huku akitaka Uongozo wa Mfuko huo kutumia TAKUKURU kudai madeni yao waliowakopesha wakulima leo Februari 18,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko wa Pembejeo Bw.Festo Mhimba,akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Husein Bashe,wakati alipofanya kikao na watumishi wa Mfuko huo huku akitaka Uongozo wa Mfuko huo kutumia TAKUKURU kudai madeni yao waliowakopesha wakulima leo Februari 18,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Husein Bashe,akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko wa Pembejeo Festo Mhimba,wakati alipokutana na watumishi wa Mfuko wa Pembejeo huku akitaka Uongozo wa Mfuko huo kutumia TAKUKURU kudai madeni yao waliowakopesha wakulima Februari 18,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Pembejeo wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Husein Bashe (hayupo pichani) wakati alipofanya kikao na watumishi hao huku akitaka Uongozo wa Mfuko huo kutumia TAKUKURU kudai madeni yao waliowakopesha wakulima leo Februari 18,2021 jijini Dodoma.
…………………
Na Alex Sonna, Dodoma
Serikali imeuagiza uongozi wa Mfuko wa Pembejeo nchini kuitumia taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Nchini (TAKUKURU) katika kudai madeni ya mikopo waliyo wakopesha wakulima kiasi ambacho kinafikia Sh. bilini 20.
Maagizo hayo yametolewa Februari 18,2021 Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Husein Bashe, wakati alipokuwa akizungumza na watumishi pamoja na viongozi wa mfuko wa Pembejeo za kilimo.
Bashe amesema kuwa mfuko huo unatakiwa kuweka nguvu katika ukusanyaji wa madeni ya mikopo ambayo wamekopesha wakulima baada ya kubaini kiasi kikubwa cha fedha kilichokopeshwa hakijarudishwa.
“Kipaumbele chenu kwa sasa lazima kiwe ni kukusanya madeni ya mikopo mliyowakopesha wakulima toka mfuko huu uanzishwe mwaka 1995 ni takribani bilioni 20 zipo nje na kiasi ambacho mmefanikiwa kukusanya hadi hivi sasa ni bilioni 10 pekee”amesema Mhe. Bashe.
Aidha Naibu Waziri Bashe, ametoa siku 14 kwa mfuko huo kuandaa mchanganuo wa kiasi cha madeni ya mikopo iliyolipwa na wanayodaiwa wakulima ili kuanza kuchukua hatua za ufuatiliaji kwa kuhusisha mamlaka nyingine.
“Nawaomba mwandikie Mkurugenzi wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo ili muwatumie TAKUKURU kudai fedha hizi kwani wao wako vizuri katika kudai madeni hawa wengine mtasumbuana tuu na mambo ya mahakamani” amesema.
Bashe ameuagiza mfuko huo kusitisha utoaji wa mikopo hadi hapo utakapofanya marekebisho ya muundo wa mfuko huo ambapo amebainisha kuwa mfuko wa Pembejeo umekuwa hauzalishi faida.
“Mfuko huu toka uanzishwe mwaka 1995 haujawahi kutengeza faida na hii ni ktokana na muundo wenu mnatoa mikopo lakini mlivyo kama siyo taasisi inayojihusisha na utoaji wa fedha” amesema.
Aidha Mhe. Bashe ameutaka mfuko huo kuvunja mikataba yote waliyoingia na makampuni binafsi ya kudai madeni hayo kwa wakulima waliokopeshwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko wa Pembejeo Festo Mhimba, amebainisha kuwa wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi kama vile mafuriko, ukame hali ambayo inachangia wakulima kushindwa kurejesha mikopo.
Vile vile amesema kikwazo kingine ni dhana potofu iliyopo miongoni mwa wakopaji kuwa fedha ya serikali ni ruzuku hali ambayo hurudisha nyuma hamasa ya urejeshwaji wa mikopo.
Ameongeza kuwa “Janga la corona pia lilisababisha wakopaji kukosa soko la mazao ya kilimo, mifugo nauvuvi kutokana na nchi nyingi kikanda na kimataifa kujifungia”amesema Mhimba.
Post a Comment