Rais Dk John Magufuli akiamuapisha Dk. Bashiru Ally kuwa Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo
Na Bashir Nkoromo, Dar es Salaam
Katibu Mkuu Kiongozi mpya Balozi Dk. Bashiru Ally ameahidi kutekeleza majukumu yake mapya kwa juhudi na maarifa, kuzingatia sheria, taratibu, kanuni, mila na desturi huku akimshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kumuamini na kumteua katika nyadhifa hizo kubwa. .
Balozi Dk. Bashiru ameyasema hayo wakati akizungumza baada ya kuapishwa na Rais Dk. Magufuli kuwa Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi katika hafla iliyofanyika leo asubuhi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na shukrani kwa Rais na kutoa ahadi hiyo, Balozi Dk. Bashiru amewaomba Watanzania kumuombea ili atekeleze majukumu yake kama yalivyo matarajio ya Rais ambaye amejipambanua kwa kupigania maslahi ya nchi, kuwapigania Watanzania hasa wanyonge na kuimarisha mawasiliano Serikalini ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Katika hafla ya kuapishwa kwa Balozi Dk. Bashiru imehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma, Naibu Spika Dk. Tulia Ackson, Mawaziri, Makatibu Wakuu na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Wakati huo huo, Rais Magufuli ameshiriki Mkutano wa 21 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika leo tarehe kwa njia ya mtandao.
Mkutano huo unaongozwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo.
Post a Comment