*KADA WA CHAMA* ni Mtu mwenye Mafunzo Maalumu kuhusu Chama, Historia na mafunzo ya ulinzi wa Chama dhidi ya Uvamizi au Hujuma yeyote.
Pia ni Mtu anayekereketwa muda wote Kukiendeleza Chama chake.
Yupo tayari Kufa kwa ajili ya kukitetea Chama Chake.
Kuwa KADA Siyo jambo la lelemama, wapaswa ujikane nafsi yako.
*SIFA PAMBANUZI ZA KADA.*
✔️Hufahamu vema Historia ya chama chake.
✔️Hufahamu vema Misingi, Itikadi, Sera na Taratibu za chama chake.
✔️Huishi kwa kufuata Misingi na Kanuni ya Chama na itikadi zake.
✔️Huwa tayari kukitetea Chama kwa Kuzingatia Maelekezo na Taratibu za Chama, Hata katika Mazingira hatari na huwa tayari kuanzisha tawi la chama popote atakapokuwa lengo ni kukipanua chama chake na siyo kukiua.
✔️Hapaswi Kukikashifu Chama chake hadharani bali anapaswa kuyarekebisha Masuala yote yenye utata katika vikao halali vya chama.
✔️Huwa na uwezo wa Kujisimamia, Mvumilivu kwa Wapinzani wa Nje na ndani na anauwezo wa kutoa suluhu za Changamoto za Chama kwa kuzingatia Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Chama.
*KADA.*
_Siyo. Mtu anayesubiri mavuno wakati wa uchaguzi Bali ni mtu anayeshiriki kikamilifu katika ujenzi na uimarishaji wa Chama, nyakati zote._
_Siyo MTU wamafumbo na uchonganishi_
_Siyo MTU wakujipendekeza Kwa maslahimaslahi_
_Ni Mtu anayetanguliza mbele maslahi ya Chama chake kwa manufaa ya Nchi na Taifa lake._
Modified By. *Goodluck N.BoSha.*
Contact. 0627799285.
Email. goodluckbosha14@gmail.com
Post a Comment