Katika maandamano hayo ya jana huko Abuja wananchi wa Nigeria walipiga nara na kulaani kuendelea kushikiliwa Sheikh Zakzaky na mkewe. Waandamanaji hao ambao walikuwa wamebeba mabango na picha za Sheikh Zakzaky wametangaza uungaji mkono wao kwa kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.
Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe walitiwa mbaroni Disemba 13 mwaka 2015 katika shambulio la jeshila Nigeria katika Husseiniya iliyopo katika mji wa Zaria nchini humo.
Vikosi vya jeshi la Nigeria siku walipomtia mbaroni Sheikh Zakzaky waliwafyatulia risasi hadhira iliyokuwa imekusanyika katika Husseiniya hiyo na nyumbani kwake na kuwauwa shahidi mamia ya watu wakiwemo watoto wake watatu.
Katika miezi ya karibuni ambapo hali ya kimwili na kiafya ya Sheikh Ibrahim Zakzaky imezidi kuwa mbaya taasisi mbalimbali za haki za binadamu mara kadhaa zimetoa wito zikitaka kuachiwa huru kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.
Post a Comment