Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Eng. Joseph Nyamhanga amemuelekeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam kuhakikisha machinjio ya vingunguti inaanza kutoa huduma mapema mwezi March,2021.
Eng. Nyamhanga ameyasema hapo alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Machinjio hiyo ya Kisasa na kubaini ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 98.
“ Ujenzi wa machinjio hii umeshakamilika kwa kiwango cha kuanza kutoa huduma sasa inatakiwa kazi zianze hata kwa kuchinja ng’ombe,mbuzi na kondoo wachache mpaka hapo mtakapokamilisha ujenzi kwa asilimia 100” Nyamhanga
Pia alieleza kuwa Machinjio za Kisasa zinajengwa katika Halmashauri 7 Nchini lengo ikiwa kuzijengea uwezo Halmashauri ziweze kujitegemea kimapato.
Alitaja maeneo ambayo Machinjio hizo zinajengwa kuwa ni Manispaa ya Lindi, Sumbawanga, Shinyanga, Songea, Mpanda, Iringa na Halmashauri ya Mji wa Geita.
"Machinjio hii ikianza kutoa huduma itakua inakusanya Bil 2 mpaka Bil 5 kwa mwaka sasa mapato hayo yatawezesha Jiji la Ilala kupunguza utegemezi kwa Serikali na kutekeleza miradi ya maendeleo na kutoa huduma bora kwa Wananchi ,"Nyamhanga.
Pia Eng. Nyamhanga aliutaka Uongozi wa Jiji hilo kuanzisha Kampuni(Special purpose vehicle) kwa ajili ya kuendesha Machinjio ya Vingunguti.
Naye Meneja wa Ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti Eng. Mburuga Matamwe amesema mradi umekamilika kwa Hatua asilimia 98 kwa kazi za ndani na za Nje.
Alieleza uwezo wa machinjio hiyo kuwa ina uwezo wa kuchinja ngombe 1,500 kwa siku huku mbuzi na kondooo ni 3000 kwa siku.
Post a Comment