Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally, akishangilia na viongzi wengine wa CCM, baada ya kukata utepe kufungua rasmi jana Maonesho ya Kihistoria ya Maadhimisho ya Miaka 44 ya CCM, yanayoendelea katika katika Jengo la White House la Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, Dk. Bashiru ameagiza maonesho hayo yaendelee hadi mwisho wa mwezi huu wa Februari, ili Viongozi, Wanachama wa CCM na Wananchi kwa jumla wayatembelee kujua kwa kina historia ya Chama.
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, akizungumza na kumkaribisha Katibu Mkuu kufungua rasmi maonesho hayo.
Shangwe kwa watumishi na Wanachama wa CCM wakishangilia baada ya Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru kufungua maonesho hayo👇
>>>>>>>>>>>
Kisha Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru akafika eneo la Maonyesho hayo👇
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru akipatiwa maelezo ya awali wakati Afisa katika Kitengo cha Nyaraka na Kumbukumbu akimkaribisha kutazama maonyesho hayo.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru akipewa maelezo kuhusu moja ya magari yaliyotumika wakati wa harakati kudai Uhuru wa Tanganyika.
Katibu Mkuu Dk. Bashiru akiangalia nyaraka na picha mbalimbali za kihistoria kwenye maonyesho hayo katika Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.👇
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akipiga 'shoto kulia' huku akiongozwa na Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole kwenda Kufungua maonyesho hayo.
Kibwagizo👇
Author Name
Author Description!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment