Mwanzilishi wa kampuni ya Amazon, Jeff Bezos amejiuzulu katika wadhifa wake wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo ya biashara ya mtandaoni ambapo nafasi yake sasa itachukuliwa na Andy Jassy, ambaye kwa sasa anaongoza biashara ya uhifadhi wa data.
Taarifa iliyotolewa na Andy Jassy imeeleza kuwa Bezos atakuwa mwenyekiti wa kampuni hiyo na atashiriki kimamilifu katika shughuli zote za kuiongoza kampuni hiyo.
Aidha Jassy ameeleza kuwa mabadiliko hayo yatafanyika katika kipindi cha nusu ya pili cha mwaka 2021.
Post a Comment