Featured

    Featured Posts

NMB YAKABIDHI MABATI 200 KWA AJILI YA UKARABATI WA MADARASA YA SHULE YA SEKONDARI JAMBIANI KUSINI UNGUJA


Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam, Donatus Richard (mwenye suti wapili kulia) akipeana mkono na Waziri wa Kilimo Maliasili na Umwagiliaji Zanzibar, Soud Nahoda Hassan wakati wa makabidhiano ya vifaa vya ujenzi vikiwemo mabati mia mbili kutoka Benki ya NMB kwa ajili ya shule ya Jambiani Sekondari. Kushoto ni Meneja Tawi la NMB Tawi la Zanzibar, Abdalla Duchi 

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam, Donatus Richard, Waziri wa Kilimo Maliasili na Umwagiliaji Zanzibar, Soud Nahoda Hassan wakifurahia pamoja na  Walimu, Wanafunzi na Wazazi baada ya Makabidhiano ya  mabati 200 na vifaa vyengine vya ujenzi kwa ajili ya shule ya Jambiani Sekondari. 

 Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam, Donatus Richard, Waziri wa Kilimo Maliasili na Umwagiliaji Zanzibar, Soud Nahoda Hassan pamoja na baadhi ya wazazi waliohudhuria hafla na makabidhiano  ya mabati 200 na vifaa vyengine vya ujenzi kwa ajili ya shule ya Jambiani Sekondari.


*******


Benki ya NMB imekabidhi mabati 200 na vifaa vyengine vya ujenzi kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa ya Shule ya Sekondari ya Jambiani, Kusini Unguja. Akizungumza katika hafla ya makabidhianao hayo iliyofanyika skulini hapo, Meneja wa NMB Kanda ya Dar-es-salam, Donatus Richard alisema wameamua kutoa msaada huo ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha sekta ya elimu.


“Benki ya NMB tumeamua kushirikiana pamoja na Jamii yote inayozunguka eneo la Jambiani kuchangia mabati 200 kwa ajili ya kutatua changamoto ya kuvuja kwa madarasa wakati wa mvua” alisema Donartus.


Aliongeza kuwa elimu ni kichocheo cha maendeleo hivyo kuna kila sababu kwa watoto kupata mazingira mazuri ya kupata elimu na kusisitiza ndio maana benki ya NMB imeamua kuisaidia skuli hiyo.


Nae Mwakilishi wa Jimbo la Paje ambae pia ni Waziri wa Kilimo, uvuvi, mifugo na umwagiliaji, Sudi Nahoda ameishukuru benki hiyo kwa msaada huo na kusema utasaidia kutatua changamoto ya kuvuja kwa skuli hiyo.


“Nikuhakikishieni kuwa msaada huu mliotupatia una thamani kubwa na kiuhalisia NMB ni moja kati ya mashirika yanayojali Jamii katika kuleta maendeleo.” Alisema Mhe. Sudi


Kwa upande wake kaimu mwalimu mkuu wa Skuli ya Jambiani, Haji Haji ameishukuru NMB kwa msaasa huo, amesema kwa muda sasa wamekuwa wakikabiliwa na ubovu wa madarasa ambapo wanafunzi wamekuwa wakishindwa kuhudhuria masomo  katika vipindi vya mvua.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana