Katibu Mkuu Dk. John Jingu akisisitiza jambo |
Sehemu ya wataalam wa maendeleo ya jamii wakisikiliza kwa makini Katibu Mkuu, Dk. Jingu akizungumza wakati wa mkutano huo.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara ya Maendeleo ya Jamii, Dk. John Jingu amewapiga msasa wataalam wa maendeleo ya jamii kwa kuwataka kupanga mikakati thabiti ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Akizungumza katika kongamano la wataalamu hao Dk. Jingu amesema kuwa uongozi wa kimkakati ni uongozi unaoleta mabadiliko, hivyo ni lazima wafanye kazi kimkakati na kwa mafanikio makubwa ya kuwaletea wananchi maendeleo.
"Kazi yenu pia ni kubadilisha fikra za watu na ili uweze kufanya hayo inabidi uwe na sifa ya kuwa na uwezo wa kujenga timu ya kufanya kazi. Huwezi kufanya kazi peke yako, hilo ni kosa na kisaikolojia ni hatari sana lakini kubwa sana kufanikisha mkakati uwe ni mtu wa kusikiliza," amesema Dk Jingu.
Dk. Jingu ametaja pia sifa zingine anazopaswa kuwa nazo kiongozi kuwa ni kusoma hisia za jamii inayomzunguka na kuziheshimu, kuheshimu mila na desturi ya jamii anayoihudumia pamoja na kujua mabadailiko anayowapelekea endapo wanayakubali ama wanayakataa.
Amewataka kuwa waadilifu, wawajibikaji na kutii miiko ya kutopokea rushwa, kutokuwa na upendeleo, ama sivyo watakosa imani katika jamii wanayoihudumia.
"Mnatakiwa kuwa na haiba nzuri inayokubalika katika jamii, walimu wana haiba yao, watumishi wa umma pia wana haiba yao hivyo mdumishe utaratibu huo, mtaheshimika," amesisitiza Dk. Jingu.
Dk. Jingu alimazia kwa kuwaasa watalaamu hao wa maendeleo ya jamii kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kwamba watakuwa huwaitendei haki jamii na taaluma yao, hivyo kuwataka kufanya kazi kimkakati kwa kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi.
Kongamano hilo lililofunguliwa juzi na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima limehudhuriwa na wataalam wa maendeleo ya jamii 400 kutoka mikoa yote nchini. Kesho wanafanya mkutano mkuu ambapia pia watafanya uchaguzi wa viongozi wa kukiongoza chama chao cha Codepata.
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video Dk. John Jingu akizungumza kwenye mkutano huo....
Imeandaliwa na; Richard Mwaikenda
Imeandaliwa na; Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
Post a Comment