RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Haji Omar Haji kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar, Ikulu Jijini Zanzibar, leo. Wapili kulia ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Khadija Shamte Mzee kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, Ikulu Jijini Zanzibar, leo. Wapili kulia ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Haroun Ali Suleiman na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi wakifuatilia kuapishwa kwa Majaji wa Mahakama Kuu Zanzibar na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, Ikulu Jijini Zanzibar.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Majaji wa Mahakama Kuu Zanzibar na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, Ikulu Jijini Zanzibar.
AHUTUBIA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR👇
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Idrisa Mustafa Kitwana, wakienda katika ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, kuhudhuria Siku ya Maadhimisho ya Sheria Zanzibar, leo. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar, yalioadhimishwa katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, leo. Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni “Wajibu wa Mahakama na Wadau wa Sheria kwa Kuendena na Kasi ya Awamu ya Nane katika Kushughulikia Kesi”.JAJI Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akizungumza katika wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar yaliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Haroun Ali Suleiman akizungumza alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuzungumza na Wanasheria katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar, katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Dk. Mwinyi Talib Haji akizungumza na kutoa Salamu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar, yaliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
NAIBU Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Muumini Khamis Kombo akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
BAADHI ya Mawakili na wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya Maadhimisho ya Siki ya Sheria Zanzibar, yaliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Post a Comment