Na Richard Mwaikenda, Dodoma
MBUNGE wa Jimbo la Makambako, Deo Sanga amesema kuwa Rais John Magufuli atake asitake ataongezewa kipindi kingine cha kuiongoza nchi.
Sanga ameyasema hayo bungeni Dodoma leo alipokuwa akichangia hotuba ya Rais Jonh Magufuli aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la 12 Novemba 2020.
Amesema kuwa kuongezewa muda wa kuongoza kwa Rais Magufuli si dhambi, kwani anatakiwa aendelee kuingoza nchi.
Baada ya Mbunge Sanga kumaliza kuzungumza, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson alisema kuwa Rais Magufuli alishatoa msimamo wake kuhusu jambo hilo, ila wabunge ni hawauiwi kuzungumzia.
Post a Comment