…………………………………….
Mabingwa wa Tanzania bara timu ya Simba SC imetwaa Kombe la Simba Super Cup licha ya kulazimishwa sare ya 0-0 na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Januari 31,2021 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo Simba SC inamaliza na pointi nne kufuatia ushindi wa 4-1 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Al Hilal ya Sudan .
Hilal ya Sudan imemaliza nafasi ya pili kwa pointi zake tatu baada ya kuichapa Mazembe 2-1 Ijumaa.
Kiungo kutoka Msumbiji, Luis Miquissone aliteuliwa Mchezaji Bora wa Mechi ya leo na kupewa Sh 500,000.
Kiungo Mzambia, Larry Bwalya aliteuliwa Mchezaji Bora wa Mashindano, wakati Mfungaji Bora ni winga Mghana, Bernard Morrison aliyepachika mabao mawili na Kipa Bora Beno Kakolanya wote waliapata Sh. Milioni 2 kila mmoja.
Post a Comment